Kila mtu nchini Uswisi ana haki ya kupokea matibabu. Katika kituo cha kimbilio, nenda kwenye Medic-Help kwanza ikiwa una dalili yoyote.
Kwanza nenda umwone daktari wako mkuu
Nchini Uswisi, daktari wako mkuu ndiye mtu wa kwanza wa kuwasiliana naye ukikabiliwa na ugonjwa au ajali. Atakutibu, na ikihitajika, atakupa rufaa kwenda hospitali au kwa daktari mwingine.
Daktari mkuu anapowajua wagonjwa wake na historia yao ya matibabu, anaweza kuwapa matibabu bora. Kwa hiyo, daima nenda kwa daktari wako mkuu kwanza.