Magonjwa

Je, umekuwa ukiugua kwa muda mrefu? Je, unameza dawa mara kwa mara? Je, ulipokea matibabu katika nchi yako asili, au ulipokua mkimbizi?

Icon_Medic_Help.png

Tembelea Medic-Help na ueleze matatizo yako.

Baadhi ya magonjwa huambukiza. Hii inamaanisha kuwa ugonjwa husika unaweza kusambaa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine. Ugonjwa unaweza kusambaa kupitia hewa, mikono michafu, damu au ngono, pamoja na matapishi, uchafu wa mwili au kugusana moja kwa moja.

Icon_Medic_Help.png

Wasiliana na Medic-Help ikiwa una dalili hizi. Hatua hii itasaidia kujilinda binafsi na watu walio karibu nawe.

Magonjwa kama vile kisonono, malengelenge, kaswende au klamidia yanaweza kuenezwa kupitia ngono. Athari zinaweza kujumuisha usaha, miwasho na uvimbe, vidonda au maumivu katika sehemu za uzazi. Hata hivyo, pia unaweza kuwa umeambukizwa lakini usiwe na dalili zozote.

Icon_Kondome.png

Jilinde dhidi ya magonjwa ya zinaa. Tumia kondomu kila unapofanya ngono. Unaweza kuzipata kituoni au kuzinunua katika duka la dawa au maduka makubwa.

Icon_Medic_Help.png

Ikiwa una dalili yoyote ya magonjwa ya zinaa, tembelea kituo cha Medic-Help.

Icon_Medic_Help.png

Ikiwa huna hakika kama umeambukizwa magonjwa ya zinaa baada ya kufanya ngono bila kondomu, nenda ukapate ushauriano kwenye kituo cha Medic-Help. Usisubiri hadi upate dalili.

HIV ni virusi vinavyodhoofisha hali ya kingamwili. Unaweza kuwa na virusi hata bila kuonyesha dalili. Ikiwa hutumii dawa, inaweza kudhoofisha mwili wako kiasi ya kwamba unaugua. Hali hii inajulikana kama Ukimwi.

Ugonjwa huu husambazwa kupitia damu, wakati wa kufanya ngono bila kondomu, kwa kutumia sindano zenye viini, au moja kwa moja kutoka kwa mama hadi mtoto ambaye hajazaliwa. Ikiwa una virusi hivi, unaweza kuwaambukiza watu wengine hata bila ya kuwa na dalili yoyote.

Ugonjwa wa HIV/Ukimwi hauna tiba. Hata hivyo, matibabu husaidia kudhibiti virusi na kupunguza madhara yake.

Icon_Kondome.png

Jilinde dhidi ya HIV/Ukimwi. Tumia kondomu kila unapofanya ngono. Unaweza kuzipata kituoni au uzinunua katika duka la dawa au maduka makubwa.

Icon_Spritze.png

Kila mara, tumia sindano safi na zisizotumiwa unapodunga dawa mishipani ili kuzuia kuambukizwa.

Icon_Medic_Help.png

Nenda upate ushauri kwenye kituo cha Medic/Help ikiwa hujui kama huenda umeambukizwa HIV/ Ukimwi au ugonjwa mwingine wa zinaa baada ya kufanya ngono bila kondomu. Usisubiri hadi upate dalili.

Watu huwa na kikohozi cha kifua kikuu kwa kipindi kisichozidi wiki tatu, wana homa, kutokwa na jasho usiku, au kupoteza uzito. Ugonjwa wa kifua kikuu unaweza kusambazwa wakati watu wenye afya wanavuta pumzi ya watu wenye ugonjwa huo wanapokohoa.

Kifua kikuu ni hatari. Hata hivyo, ugonjwa huu unaweza kutibiwa ukitambuliwa katika awamu za kwanza. Matibabu yake huchukua muda usiopungua miezo sita.

Icon_Medic_Help.png

Ikiwa una dalili za kifua kikuu, tayari umetibiwa kifua kikuu mara moja au ulikuwa karibu na mtu aliye na ugonjwa huu, tembelea kituo cha Medic-Help.

Pombe, dawa za kulevya na nyinginezo zinaweza kukutawala na kuharibu afya yako. Epuka kutumia dawa za kulevya.

Magonjwa yanaweza kuambukizwa kupitia damu wakati wa kudungia dawa za kulevya mishipani, kwa mfano, sindano zinapotumiwa tena.

Icon_Spritze.png

Ikiwa huwezi kuepuka dawa za kulevya, tumia sindano safi na zisizotumiwa awali kila mara ili uepuke kuambukizwa.

Icon_Medic_Help.png

Uraibu wa dawa za kulevya unaweza kutubitiwa au kudhibitiwa. Wasiliana na Medic-Help.

Vurugu au matukio magumu - kama vile vita, kutoroka, kuteswa na kubakwa - yanaweza kusababisha ugonjwa wa mwili au akili. Kulewa pombe kwa wingi au vileo vinginevyo pia kunaweza kuchangia.

Watu wengi walioathirika hushindwa kuzungumza kuhusu magonjwa ya akili. Ni muhimu kuwachukulia kwa makini na kuwatafutia matibabu kama vile wagonjwa mengine tu.

Dalili za magonjwa ya akili zinazoweza kutokea ni pamoja na kutoweza kulala vizuri kwa muda mrefu, kutoa majinamizi, maumivu yasiyoeleweka au matatizo mengine.

Icon_Medic_Help.png

Dhiki ya kiakili inaweza kutibiwa. Wasiliana na Medic-Help.

Tetekuwanga ni ugonjwa unaoambukiza kwa viwango vya juu. Dalili za kawaida huwa homa na vipele vya ngozi na viputo visivyo na rangi katika awamu za awali. Unaweza kujilinda dhidi ya tetekuwanga kwa kupokea chanjo.

Icon_Medic_Help.png

Ikiwa wewe au mtoto wako ana dalili zozote za tetekuwanga, tembelea Medic-Help.

Icon_Medic_Help.png

Ikiwa bado hujaambukizwa tetekuwanga, nenda uchanjwe. Tembelea Medic-Help.

Watu wenye surua mara nyingi huwa na homa, macho mekundu, kikohozi na vipele vya ngozi na madoa mekundu. Unaweza kujilinda dhidi ya surua kwa kupokea chanjo.

Icon_Medic_Help.png

Ikiwa wewe au mtoto wako ana dalili zozote za surua, tembelea Medic-Help.

Icon_Medic_Help.png

Ikiwa bado hujaambukizwa surua, nenda uchanjwe. Tembelea Medic-Help.

Dondakoo ni ugonjwa wa ngozi au njia za pumzi za sehemu ya juu. Kuna aina mbili za ugonjwa huu: ugonjwa wa koo na wa ngozi.

Watu wenye ugonjwa huu wa koo mara nyingi hukabiliwa na maumivu ya koo, homa na maumivu wakati wa kumeza. Dalili kuu zaidi za dondakoo la ngozi ni vidonda ambavyo haviponi vizuri. Unaweza kujilinda dhidi ya dondakoo kwa kupokea chanjo.

Icon_Medic_Help.png

Ikiwa wewe au mtoto wako ana dalili zozote za dondakoo, tembelea Medic-Help.

Icon_Medic_Help.png

Ikiwa bado hujaambukizwa dondakoo, nenda uchanjwe. Tembelea Medic-Help.

Upele ni ugonjwa wa ngozi unaoambukizwa sana. Ugonjwa huu huanzishwa na vimelea vinavochimba ngozini.

Dalili za mwili hujumuisha miwasho mikali, chunusi na vipele vya ngozi, hasa katika sehemu za uzazi, katikati ya vidole, kwenye vifundo vya mikono na viungo vingine, chini ya mikono kwenye chuchu. 

Ugonjwa juu huambukizwa kupitia kugusana ngozi moja kwa moja baina ya watu wawili.

Icon_Medic_Help.png

Ikiwa wewe au mtoto wako ana dalili zozote za upele, tembelea Medic-Help.

Tumbo na matumbo yanapovimba, kichefuchefu, kutapika na kuharisha hutokea, pamoja na homa na maumivu ya tumbo. Watu walio na ugonjwa huu mara nyingi hupoteza maji mengi mwilini kwa muda mfupi.

Icon_Medic_Help.png

Ikiwa una dalili yoyote ya uvimbe wa matumbo, tembelea kituo cha Medic-Help.

Icon_Trinken.png

Kunywa maji au chai ya kutosha kwa kiasi kidogo.

Icon_Haende_waschen.png

Nawa mikono yako mara nyingi kwa sabuni ili uepuke kuwaambukiza watu wengine.

Kuna magonjwa mengine mengi. Hapa utapata maelezo zaidi kuhusu magonjwa makuu ya kuambukiza.

Icon_Medic_Help.png

Tembelea Medic-Help hata kama dalili zako hazifanani na za magonjwa yaliyoelezwa hapa.